Ajali hii ilitokea nchini Uingereza ambapo dereva wa lori kubwa la mafuta lililokuwa linakwenda kwa spidi ya kilomita 96 kwa saa anadaiwa kutogundua kuwa alikuwa akiliburuza gari dogo aliloligonga ambalo lilinasa kwenye boneti lake la mbele. Bonyeza PLAY kushuhudia mwenyewe ajali hiyo ya kushangaza...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete (kulia), pamoja na Mama Salma Kikwete(katikati), wakijiandikisha kama wapiga kura katika kijiji cha Msoga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, Machi 3, 2010.
Na Walusanga Ndaki UBORESHAJI wa Daftari la Wapiga Kura nchini kwa jiji la Dar es Salaam unaanza tarehe 22 Machi, mwaka huu Jumatatu kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)...
Baada ya Kocha wa Simba Mzambia, Patrick Phiri kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, huku Kocha wa Yanga Kosta Papic akionekana kuleta mapinduzi katika soka la wachezaji wa Yanga, kumeibuka ushindani kwa mashabiki kuwa nani ni mkali kati yao...
Timu ya taifa ya wanawake ya mpira wa miguu ‘Twiga Stars’ jana ilipata nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano ya kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Huru ya Afrika baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Ethiopia, katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Awali timu hizo zilikipiga nchini Ethiopia, ambapo Twiga Stars iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, hivyo sare ya jana iliifanya Twiga kuongoza kwa ushindi wa jumla ya magoli 4-2, na hivyo kusonga mbele katika michuano hiyo ambapo sasa inatarajiwa kumenyana na Eritrea.
Kikosi cha Twiga Stars kilichoiua Ethiopia.
Kikosi cha Ethiopia kilichochapwa.
Sehemu ya mashabiki walihudhuria mpambano huo.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika (mwenye suti)
Kiungo mshambuliaji wa Twiga Stars, Ester Chabruma a.k.a Lunyamila (kulia) akimtoka kwa staili ya kumruka beki wa Ethiopia, Tiruanch Imengsha Sisay.
Beki na Nahodha wa Twiga Stars, Sophia Mwasikili (katikati) akiwadhibiti washambuliaji wa Ethiopia, Eden Shiferaw Negeri (kushoto) na Semira Kemar Aman.
Ester Chabruma wa Twiga Stars akimtoka Semira Kemar Aman.
Wachezaji hawa wa Simba na Yanga, nao walikuwepo Uwanjani kushuhudia mtanange huo, kutoka kushoto ni golikipa wa Simba, Juma Kaseja, Kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari na Mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi.
Wachezaji wa Twiga Stars, wakishangilia baada ya kupata bao.
Polisi ilibidi waingie uwanjani baada ya Ethiopia kuanza kufanya fujo wakikataa bao walilofungwa, mpaka mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa ni sare ya 1-1.
Wachezaji wa Ethiopia wakilia baada ya kufungwa na mpira kumalizika.
Waziri wa Maendelea, Jinsia, Wanawake na Watoto, Margreth Sitta (mwenye cheni) akiwa na tabasamu pamoja ya kikosi cha Twiga baada ya ushindi huo.
..mwanamuziki aliyejipatia umaarufu afrika mashariki katika siku za karibuni, Kidumu, usiku wa kuamkia leo aliibukia academy ya wadau wa muziki iliyoko Kunduchi Beach Hotel na kutoa burudani fupi kwa kuimba wimbo wake wa Haturudi Nyuma kwa kushirikiana na kundi la THT lililokuwa likitoa burudani. ...Kidumu (kati) akiwa na Saida Kessy wa Clouds FM akiwa na ankal michuzi ..wadau wa muziki wakiachia na burudani..
..Gadna G (kutoka kushoto), Ruge wakiongea na Kidumu huku MD wa One plus Comm, Fina Mango (kulia) akisikiliza
...wasanii wa THT wakitoa burudani..
..msanii wa THT Dogo Ditto (kulia) akimpelekesha kwa burudani Lady Hanifa wa Radio One/ITV
... mdau na mlezi wa wasanii Tanzania, Dotnata (kushoto), akiwa na Mumewe Shaaban Posh (kulia) na ankal michuzi PICHA: Abdallah Mrisho/GPL
Ndugu Wanabidii kumezuka Ujambazi wa ajabu hapa Jijini Dsm. Juzi tarehe 17//3/2010 Jirani yangu alikwenda Benki kuchukua pesa majira ya saa 10:00 jioni Mjini. Baada ya kuchukuwa pesa zake alielekea kituo cha Basi kusuburi Basi. Akiwa kituoni hapo akashtukiwa mama mmoja anamfuata na kusema ndiye huyu. Wakajitokeza na wanaume wengine wakamkamata yule mama akasema
..David Minja kutoka TBL akifafanua jambo kufuatia hoja zilizotolewa na wadau wakati wa kujadili categories na vigezo
..Mpoki wa Orijino Komedi nae ni miongoni mwa wadau wa semina ya leo
..Efraim Mafuru kutoka Vodacom, (kulia), wadau Hartman, Abdul Tall na Khadija Kalili kutoka Tanzania Daima
...wadau wa muziki kutoka kushoto: Baucha wa Baucha Records, Mkallah Fundikira kutoka Royal Production na Raphael Chambo 'DJ Rachy' kutoka Club La casa Chika, Tanga.
..ankal Michuzi (kushoto) akiwa na mdau Mboni Masimba ndani ya semina
Mchana huu kunafanyika semina ya kuanza mchakato wa kuwatafuta wasanii bora wa muziki wa kizazi kipya na wasanii wengine wa Tanzania (Tanzania Music Awards 2010). zifuatazo ni baadhi ya picha za wadau wanaohudhuria semina hii:
Kunduchi Beach Hotel..lango kuu
...ndani ya ukumbi wa semina
..Frank Mtao (kulia) kutoka Two Eyez production
..Salma Msangi (kushoto) mtangazaji wa Channel ten
..watangazaji wa TV na Redio ..Sauda Mwilima (kushoto), Maimartha Jesse (kulia), Dina Marios (kushoto mwa Sauda).
..Dotnata (kushoto) na Dina wakipeana michapo..
..Matangazaji wa Clouds FM B12(kushoto) na Luca, kutoka mtandao na jarida la Bongo5
...Mtangazaji wa Radio One, Millard Ayo (kushoto), Sauda na Dotnata
Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka nchini Burundi ambaye zaidi shughuli zake za muziki anazifanyia nchini Kenya, Amosozi V’urukundo ‘Kidumu’ usiku wa kuamkia leo alifanya makamuzi ya hatari ndani ya Club Sun Cirro ya jijini Dar es Salaam na kuwapagawisha vilivyo mashabiki waliofurika ukumbini hapo. Kidumu yupo nchini tangu jana na aliletwa Bongo kwa udhamini wa Hartman Production na EATV.
Kidumu akifanya makamuzi yake ndani ya Club Sun Cirro usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya waimbaji wake wakionesha uwezo wa kukata nyonga katika onesho hilo.
Mmoja kati ya mashabiki ‘waliotia maguu’ ukumbini hapo akipewa mic na Kidumu ili ajaribu kuimba wimbo wowote anaoufahamu.
Baadhi ya Mashabiki waliohudhuria shoo hiyo wakichizika kwa burudani zilizokuwa zikitolewa na msanii huyo.
Kidumu akipiga drum kwa utaalamu wa hali ya juu huku akiimba,kitu kilichozidi ‘kuwamaliza’ mashabiki wake.
Wakazi hawa wa jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo wamenaswa na kamera yetu wakiserebuka katika onesho la Bendi ya Akudo Impact, lililofanyika katika Ukumbi wa Mango Garden uliopo Kinondoni, jijini Dar kama vile wako kwenye sikukuu.
ZE BINGWA NA KIBEGI CHA MTOTO JUKWAANI Rapa wa Bendi ya Akudo Impact, Totoo Ze Bingwa usiku wa kuamkia leo amenaswa na kamera yetu akipanda jukwaani na kibegi cha mtoto, staili ambayo ilipondwa na baadhi ya mashabiki na kusema huo ni ‘ubishoo’ usio na maana kwani atachakaza kibegi cha shule cha mtoto. Ishu hiyo ilikuwa ni ndani ya ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni kwenye onesho la Akudo.
BABA’AKE UTAIBWA Njemba huyu alinaswa akiwa ameutandika usingizi wa pono kwenye kiti alichokuwa amekalia, katika onesho la Akudo lililofanyika usiku wa kuamkia leo.
• Ni matokeo ya 'mabao' ya sh 3000 wanayopiga daladala, teksi RUSHWA ndogondogo za barabarani zimewanufaisha baadhi ya askari wa Usalama Barabarani, jijini Dar es Salaam (trafiki) ambao wanakusanya zaidi ya sh 10,000,000 kila siku kila mmoja, kutokana na mchezo wa kupokezana fedha (upatu) waliouanzisha hivi karibuni...
Na Mwandishi Wetu The Supermodel, aliye pia Miss Tanzania 10 Bora 2008-09 anayedaiwa kufanyiwa unyambilisi wa kubakwa kisha kupigwa picha chafu, anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine, hii ikihusu kukamatwa kwa mtuhumiwa wa ubakaji huu...
Na Mwandishi Wetu Ndugu Lawama, huo ni wimbo kutoka bendi marehemu ya Double M Sound, lakini una maana kubwa katika jamii zetu, na imethibitika kwenye ndoa ya wasanii wa filamu nchini, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ na Wastara Juma kutokana na dhoruba zito linalowapiga...
Na Richard Bukos Mrembo aliyewahi kuwa gumzo kupitia uhusiano wake wa kimapenzi na wanasoka wawili kwa nyakati tofauti, kipa timu ya Simba, Juma Kaseja na kiungo wa Yanga, Athumani Idd Chuji, zote za Dar es Salaam, Jamilah Hassan, hatimaye amechumbiwa...